Mwenzenu nimejionea maajabu
kwenye uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya Katiba ngazi za wilaya.
Jaji Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Tanzania, Joseph Warioba
Miongoni mwa wagombea wa
nafasi hiyo, waliofika mbele ya Kamati ya maendeleo ya Kata ya Tabata
inayoongozwa na diwani mwanamama Mtumwa, ni pamoja na wakili wa kujitegemea.
Bila shaka, alikusudia
kutumia taaluma yake kuchangia mchakato wa taifa kujikwamua na changamoto
nyingi zinazolikabili. ha! kwani Kamati ilijali uanasheria?! Hakuchaguliwa bwana!
Waliochaguliwa kwa haraka ilibainika kuwa sifa ya
kwanza na ya msingi ni wana chama kimoja tu. Kila mtu sasa anahoji ikiwa
kinachokwenda kufanywa ni kupitia rasimu ya Katiba chama hicho au ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania?
No comments:
Post a Comment