Chiku Abwao, viti maalumu (Chadema) anasema
matusi, vurugu bungeni na kutikiswa kwa amani nchini kunatokana kunatokana na
Chama Cha Mapinduzi, ambacho ni chama cha siasa kikongwe kuliko vyote nchini,
kutosikiliza vilio vya wananchi.
Anasema wabunge wa kambi ya upinzani wanapoingia
bungeni na kuwasilisha kiliio cha wapigakura wake, anazomewa, anabezwa na
kuonekana hasemi lolote; matokeo yake nao wanajibu mapigo ndiyo maana bunge
linaonekana kama ilivyo sasa.
(tofauti na zamani, sasa bunge limegubikwa na
matumizi ya lugha za kukera na matusi hali inayosababisha kudhalilisha wahusika
na taifa kwa ujumla)
Abwao anasema matukio ya watu kung’olewa kucha,
meno na kujeruhiwa kwa namna tofauti kwanini yanawapata wanaoonekana kukosoa
utendaji wa serikali?
Anasema hali hiyo ikihusishwa na hali iliyopo
bungeni ambapo watu wanakosa uvumilivu hadharani kiasi cha hicho, inatia shaka
watu hao wanapokuwa nje ya hadhara wanaweza kutenda mangapi.
No comments:
Post a Comment