Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza kwenye mkutano na Kamati ya Bunge ya masuala ya UKIMWI |
Mkurugenzi wa Mfuko
wa Akiba wa PPF, William Erio akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge, ya
masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya leo, katika makao makuu ya mfuko huo
jijini Dar es Salaam.
Mfuko huo kwa miaka
10 umeelezwa kutumia Sh. Bilioni 3 kusomesha watoto waliofiwa na wazazi wao,
ambao walikuwa wananchama wake na tangu Januari mpaka Juni mwaka huu, Sh
milioni 615 zimetumika kusomesha yatima 1,151; kuanzia chekechea hadi kidato
cha nne.
Mwakani, mfuko huo
utaongeza ufadhili huo kwa kusomesha watoto wa aina hiyo mpaka kidato cha sita.
Erio anaomba Kamati
hiyo katika shughuli zake iongeze na kazi ya udhibiti wa dawa za kulevya,
kwakuwa anaamini sasa ni janga la kitaifa hususan kwa watu walio katika rika la
ujana.
No comments:
Post a Comment