Wednesday, March 20, 2013

GREYSON NA HEAVEN


  Greyson na Heaven bwana! Njia ya walemavu ndani ya Malaika resort  wao wakageuza mahala pa kuchezea.

Sasa hii alama ya vidole vyao sijui ndo mambo Fulani?!
Greyson, Heaven (mtoto wa Pendo Paul Ndovie aliye katikati) na Godfrida  afisa habari wa TAMWA wakiwa ndani ya hotel ya Malaika jijini Mwanza.
                                                                                   Namimi nilikuwepo Malaika

Monday, March 18, 2013

                                Umeona eeh!
            Hapa siyo kwenye pango, ni ndani ya hoteli
                    Witney ndani ya Malaika Hotel
                        Pendo ndani ya Malaika hotel
                           Malaika Beach Resort – jijini Mwanza
Pendo Paul Ndovie akiwa na best wake Witney; kwenye hotel ya Malaika jijini Mwanza
Balozi wa utepe mweupe wa uzazi salama kitaifa na kimataifa, Stara Thomas (aliyeshika simu) akiwa jukwaani kwenye uwanja wa Nyamagana siku ya maadhimisho ya uzazi salama, Ijumaa iliyopita yaliyofanyika jijini Mwanza.
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Rashid Seif (aliyevaa miwani) aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uzazi salama nchini, Ijumaa wiki iliyopita akiwa jukwaani kwenye uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.
Mratibu wa utepe mweupe wa uzazi salama kitaifa na kimataifa, Rose Mlay akizungumza kwenye kutano wa wadau uliyofanyika Mwanza hoteli, Alhamis iliyopita ikiwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya uzazi salama duniani ambayo kitaifa yalifanyika jijini humo, Ijumaa iliyopita.

Mratibu wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama nchini, Rose Mlay akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya uzazi salama duniani, ambayo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza kwenye uwanja wa Nyamagana; Ijumaa iliyopita.

Chezea Stara Thomas wewe! Hapa anacheza kiduku na watoto jijini Mwanza, baada ya kuwapa elimu ya uzazi salama wakazi wa Buhongwa; ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Utepe mweupe wa uzazi salama duniani, ambayo kitaifa yaliadhimishwa jijini Mwanza Ijumaa iliyopita

Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dk. Rashid Seif akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa afya, uliyofanyika Mwanza hoteli wiki iliyopita ambako alikuwa mgeni rasmi; ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya utepe mweupe wa uzazi salama.

Thursday, March 14, 2013


 
 
 
 
 
 
 
Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania, waliotokea makao makuu Dar es Salaam; wakiwa ofisini kwa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Bangi (aliyekaa nyuma ya meza yenye mafaili mengi) wakipanga mikakati ya kufanikisha siku ya maadhimisho ya uzazi salama duniani, kitaifa mwaka huu yanaadhimishwa kesho jijini Mwanza.

SALUM Charles (8) anayesoma darasa la kwanza shule ya Msingi Nyamagana, jijini Mwanza bila kufahamu kuwa anaozungumza nao ni madaktari, (Dk. Koheleth Winani na Dk. Ahmed Makuwani) akieleza kuwa anasoma kwa bidii ili baadaye awe Daktari atakayefundisha watu wasiugue ovyo. Madaktari kwa furaha walimpa Sh 3000 akanunue kalamu na daftari wakimtia moyo aongeze bidii ili atimize ndoto zake.

MANAMZIKI nguli nchini, ambaye pia ni Balozi wa Muungano wa Utepe Mweupe nchini na ulimwenguni, Stara Thomas akiwa jijini Mwanza kama unavyomuona, 'akikamata' ugali kwa samaki.

Sunday, March 10, 2013

JICHO LA KIBANDA JAMANI!

Haya sasa furahieni! Si ndivyo mlivyotaka mtoto wa wenzenu awe mlemavu? Aishi maisha yake yaliyobaki akiona kwa kutumia jicho moja? Furahieni basi!!!

Lakini mjue hukumu ya Mungu inawangoja. Hakina sina maneno yanayotosheleza kuwaelezea; kiasi gani mnakera.

Imefika wakati watu wanatamani kuwa wakimbia nchi yao? Mnaipeleka wapi Tanzania?

Hivi Absalom Kibanda, Dk. Steven Ulimboka, Saed Kubenea, Ndimara Tegambwage, Frederick Katulanda, Richard Mgamba na wengine wenye ushahidi kwamba wanatishiwa maisha na “watu wasiojulikana” wakiomba hifadhi nchi yoyote duniani;

Tanzania itabaki kwenye ramani ya nchi zenye ambani duniani? 

Hapo tunaweka kando vifo vilivyogubikwa utata vya kama vile cha Hayati Richard Massatu  na vingine vinavyodhaniwa kuwa vilitekelezwa wakati wa giza wakati kumbe ilikuwa hadharani tena mchana kweupe mbele ya macho za watu; kama kilichompata Hayati  Daudi Mwangosi.

Hivi amani inayohubiriwa, inayoagizwa kulindwa kwa nguvu na gharama zote ni ipi? Ni lini, wenye dhamana ya kusimamia amani watafumbua macho, kuona kuwa wajibu walioupokea kwa mikono miwili unamomonyoka mithiri ya barafu lililowekwa juani?

Nini kinasubiriwa kitokee, ili hatua zichukuliwe na zionekane machoni pa umma kuwa zinalengo la kukomesha uovu unaotendwa na makundi fulani, kwa maslahi yao binafsi na si kwa taifa?

Ndiyo, ni kwa maslahi binafsi kwa sababu ingekuwa ni kwa maslahi ya taifa, vyombo vya kutetea maslahi ya aina hiyo; mathalan mahakama na mamlaka zinazosimamia taaluma nchini zipo, kwanini zisitumike?

Kwanini iwe kukomoana kwa kunyofoa viungo, kupigana na hata kuripua kwa mabomu raia wasio hatia kwa mujibu wa sheria za nchi; kisa kundi moja lina uwezo wa kifedha au dhamana kuliko jingine?
Inaboa sana aisee! Achene hizo.