Novemba 1 mwaka, huu Tume ya Mabadiliko ya
Katiba ilitimiza miezi 18 tangu ianze kazi za kuratibu mchakato wa Katiba. Ni wakati
ambao ilitarajiwa iwe imewasilisha rasimu ya pili ya Katiba, kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano na Rais wa serikali ya Zanzibar.
Hatua hiyo haijatekelezwa, kutokana na ombi la
tume hiyo kuongezewa mwezi mmoja, ili kukamilisha kazi hiyo na kuikabidhi kwa
mamlaka husika. Hata hivyo, kumeibuka taarifa kwamba wajumbe wengi wa tume hiyo,
wapo hatarini kiafya.
Hatari hiyo inaelezwa kutokana na ufinyu wa
muda, ambao umepangwa bila kutilia maanani taratibu za kiafya, ikizingatiwa
kuwa wengi wa wajumbe wa tume hiyo ni wenye umri usiopungua miaka 60
Kufuatia tetesi hizo, tukafuatilia ratiba ya
utendaji wa tume hiyo, katika hatua inayotekelezwa;
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba |
Kuboresha rasimu ya Katiba,
kwa kutumia maoni yaliyotolewa na mabaraza ya Katiba ya wilaya zote nchini,
taasisi, asasi na jumuiya zenye mtazamo unaofanana zisizopungua 600
Naibu Katibu wa tume, Casmir Kyuki anasema,
“Tunafanya kazi siku zote za kazi including (ikiwamo) Jumapili, vikao vinaanza rasmi Saa 3: asubuhi mpaka Saa 7: tunapumzika kisha Saa 9: tunaendele; kumaliza inategemea na kundi limemaliza saa ngapi kwasababu wamegawanywa katika makundi; kwa mfano jana kuna walioondoka Saa 5: usiku.”
“Tunafanya kazi siku zote za kazi including (ikiwamo) Jumapili, vikao vinaanza rasmi Saa 3: asubuhi mpaka Saa 7: tunapumzika kisha Saa 9: tunaendele; kumaliza inategemea na kundi limemaliza saa ngapi kwasababu wamegawanywa katika makundi; kwa mfano jana kuna walioondoka Saa 5: usiku.”
Daktari wa
Afya ya binadamu, Dk. Joseph Masanja anasema mtu mwenye umri wa kuanzia miaka
60 anapolazimika kufanya kazi ya kutumia zaidi akili, inatakiwa pamoja na mambo
mengine, muda wa kufanya kazi uwe kati ya Saa Nne hadi Sita kwa siku; wenye
umri chini ya huo wanaweza kufanya kazi kati ya Saa Sita hadi Nane kwa siku.
“Mazingira wanayofanyia
kazi yanatakiwa yasiwe na viyoyozi (AC), kama ni lazima basi umakini
unahitajika katika kuvitumia; Kinyume chake wataugua vichomi, (Pneumonia),” Dk.
Dk.Masanja alisema
Dk.Masanja anasema
kwa umri huo, mwili wa binadamu unakuwa katika hatari ya kushambuliwa na
magonjwa, wengi wanakuwa wanaugua Kisukari
na Shinikizo la damu; kutozingatia umri, aina ya kazi na mazingira ni kuchochea
magonjwa zaidi kwa muhusika.
“…, miili haishughulishwi vya kutosha, wafanye mazoezi sana ili mafuta
yasijikusanye na kuganda kwenye mishipa, hali inayoweza kusababisha shinikizo
la damu na hata kupooza mwili,” alieleza Dk. Masanja
Wajumbe hao
wanaelezwa pia kuwa katika hatari ya kuugua ugonjwa utokanao na uchovu (fatique). Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na mtu kuwa na hasira za haraka, kukosa hamu ya
kulala, kutolala usingizi vya kutosha au kukosa kabisa usingizi na mwili
kuchoka.
Hata hivyo, mjumbe
wa tume hiyo, Joseph Butiku alisema, “Fatigue ipo kila mahala, hata wewe
unayetafuta na kuandika habari unaweza kuugua, hapa tunafanya kazi zetu kama
kawaida tu, watu wengine wanapenda kukuza mambo.”
Jumamosi
iliyopita, tulifika nyumbani kwa Mjumbe mwingine wa tume hiyo, John Nkolo,
kumjulia hali baada ya kuugua akiwa kazini wilayani Sengerema, wakati tume ikiratibu
maoni ya mabaraza ya Katiba ya wilaya.
Naibu Waziri wa Afya nchini, Dk. Seif Rashid |
Baadaye uchunguzi
wa madaktari ulibaini kuwa Nkolo, alipatwa na ugonjwa wa kupooza upande wa
kulia; usoni na kwa maelezo ya mke wake, Joyce John, Daktari alisema ni bahati
nzuri kwamba ubongo wake haukuathiriwa na ugonjwa huo.
Sasa anafanya mazoezi ya viungo, ingawa hajaweza kuzungumza vizuri
Sasa anafanya mazoezi ya viungo, ingawa hajaweza kuzungumza vizuri
Wiki mbili
zilizopita, ziiliibuka tetesi kuwa afya ya Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph
Warioba siyo nzuri na kwamba alikuwa nje ya nchi, kutibiwa.
Tulimpigia simu
yake ya kiganjani, ikapokewa na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mke wake,
akasema Jaji alikuwa nje ya nchi lakini hakuwa tayari kutaja nchi gani.
Mahojiano kati
ya Mwandishi na Makamu mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Augustino Ramadhan, juu
ya tetesi hizo yalifanyika hivi;
Mwandishi: Tuna taarifa kwamba afya ya mwenyekiti siyo nzuri, yupo nchini
India akifanyiwa uchunguzi tunaomba kufahamu anavyoendelea.
Jaji Ramadhan: Eeeeh, mimi nipo Iringa, ila ni kweli
mwenyekiti yupo India for checkup, (kuchunguzwa afya)ebu wasiliana na Katibu
anaweza kukupa ufafanuzi zaidi.
Katibu wa
tume, Assa Rashid hakupokea simu yake ya kiganjani kila alipopigiwa hali
iliyosababisha atafutwe makamu wake,Casmir Kyuki;
“Nani
amewaambia mwenyekiti yupo India?, Aliyewapa hizo taarifa kwanini asiwathibitishie?
Kwani wewe ukienda Agha Khan kuonana na daktari, utakuwa mgonjwa?” alihoji
Kyuki na kuendelea
“Yule (Jaji
Warioba) kwa wadhifa wake (waziri mkuu mstaafu)anahudumiwa na serikali kuu na kwa
umri wake siyo ajabu kuwa na utaratibu wa kufanyiwa checkup kila baada ya muda fulani,
siyo mpaka augue; kwahiyo ikiwa yupo India labda ameenda kwa ajili hiyo.”
Mjumbe mwingine
wa tume hiyo, Dk. Edimund Mvungi anasema, “Sioni kwanini mtu afiche ukweli
uliyo wazi, tunafanya kazi kwa kasi ya ajabu; binafsi huwa naingia ofisini saa
12:45 kutoka inategemea muda wa kumaliza vikao…, wakati naingia tume nilikuwa
na tatizo la Kisukari, Pressure imenianza nikiwa humu,” anaeleza Mvungi
Utafiti umebaini
kuwa kwa muda wote huo, sera ya tume hiyo haina bima ya afya ya watendaji wake,
mtu anapougua anatakiwa kujihudumia kisha kupeleka madai ili alipwe.
Hoja ya msingi hapa ni; Watanzania watapata
Katiba itakayowaletea matokeo wanayoyatarajia?
Tukutane Juma lijalo, ambapo tutakuletea athari za hali hii katika ufanisi wa
kazi.